

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemteua Prof.Abdi Talib Abdalla kuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi.
Kabla ya uteuzi huu, Prof. Abdi alikuwa Profesa Mshiriki katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).Kwa mujibu wa taarifa rasmi, uteuzi huu umeanza rasmi Oktoba 3, 2025.