
Kinda chipukizi Estêvão ameibuka shujaa wa Chelsea baada ya kufunga bao la dakika za majeruhi lililoipa The Blues ushindi wa mabao 2–1 dhidi ya mabingwa watetezi, Liverpool, katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliopigwa usiku huu kwenye dimba la Stamford Bridge, London.
Chelsea walianza mchezo kwa kasi na walipata bao la kuongoza dakika ya 14 kupitia kiungo wao Moisés Caicedo, aliyemalizia kwa ustadi mpira wa kona uliopigwa na Cole Palmer. Liverpool walijibu mashambulizi kwa nguvu, wakitawala sehemu ya kiungo na kufanikiwa kusawazisha kupitia Cody Gakpo dakika ya 62 baada ya makosa ya safu ya ulinzi ya Chelsea.
Mchezo huo uliokuwa wa ushindani mkubwa uliendelea kwa kasi hadi dakika za mwisho, huku Chelsea wakionekana kuhitaji matokeo zaidi ili kuondoka na pointi tatu muhimu. Dakika ya 90+6, kinda mwenye kipaji kutoka Brazil, Estêvão, alimalizia pasi safi kutoka kwa Palmer na kuipatia Chelsea bao la ushindi lililolipua furaha kwa mashabiki waliokuwa wamejaa Stamford Bridge.
Hata hivyo, ushindi huo haukukosa drama kocha wa Chelsea, Enzo Maresca, alionyeshwa kadi nyekundu baada ya malalamiko makali kwa mwamuzi, na kufanya hii kuwa mechi ya tano mfululizo kwa Chelsea kuhusishwa na kadi nyekundu, safari hii ikimkumba kocha badala ya mchezaji.
Kwa matokeo hayo, Chelsea wamepanda hadi nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 11 baada ya mechi saba, huku Liverpool wakisalia nafasi ya pili wakiwa na pointi 14 na wakishindwa kurejea kileleni mwa ligi.
Mashabiki wa Chelsea sasa wanaanza kuona mwanga mpya chini ya Maresca, huku Estêvão akizidi kujijengea jina kama moja ya vipaji vinavyoibuka kwa kasi barani Ulaya.
FT: Chelsea 2–1 Liverpool
14’ Caicedo
62’ Gakpo
90+6’ Estêvão
Enzo Maresca (Chelsea Coach)
#BREAKING: TAMKO KALI la JWTZ KUHUSU TAHARUKI MTANDAONI WANAOLIINGIZA JESHI KWENYE MAMBO ya SIASA…