
Na Khadija Kalili
WAZAZI wa wanafunzi wanaohitimu elimu ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kassinga iliyopo maeneo ya Msangani Wilayani Kibaha Mkoani Pwani wameaswa kuwa walinzi wa vijana hao ambao watarudi majumbani mwao mara baada ya kumaliza mitihani yao shuleni hapo.
“Nendeni mkawalinde hawa vijana ili waweze kutimiza ndoto zao wasije kujiingiza katika makundi ya wauza dawa za kulevya,bangi na makundi mengine yenye tavua zisizo faawala kukubalika katika jamii yetu” amesema Dkt. Msuya.
Akizungumza kwenye mahafali yaliyofanyika katika viwanja vya Shule hiyo aliyekua mgeni rasmi Dkt. Daniel Cleopa David Msuya amesema kuwa vijana hao wasiachwe huru ili kuwaepusha kujiingiza katika makundi mabaya.
Dkt.Msuya amesema hayo tarehe 4 Oktoba 2025 kwenye mahali ya 13 ya shule hiyo.
Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake mwanafunzi Geofrey Petro ameeleza baadhi ya changamoto shuleni hapo kuwa ni wazazi kutolipa ada kwa wakati, kutorudisha wanafunzi kwa wakati na upungufu wa vifaa vya michezo mwisho amesisitiza kwamba Shule hiyo imefanikiwa kufanya vizuri kwa kushika nafasi ya tisa 2024 na kwamba wamo nani ya Shule 10 bora.
Dkt. Msuya ameahidi kutoa jozi mbili za vifaa vya michezo shuleni hapo huku amewasisitiza kupandisha ufaulu na washike namba moja ndani ya Mkoa wa Pwani.
“Wazazi watieni moyo waalimu lipeni ada kwa wakati na kwa kufuata utaratubu ulioekwa ambao ni mzuri kwamba kwa mwaka mnalipa kwa awamu nne”.
Dkt. Msuya amewaasa Waalimu kuepuka kutumia lugha mbaya na kutokomeza ukatili kwa wanafunzi hata kama watakua wamekosea tukomeshe ukatili ndani ya nchi yetu kumbuka ukimfanyia mtoto wa mwenzako ukatili na wa kwako atafanyiwa hivyo tuwavumilie pale wanapotukwaza mimi nasema haya kwa sababu ni Balozi wa amani”amesema Msuya.
Viongozi wengine waliohudhuria mahafali hayo ni Afisa Elimu TaalumaSekondari Kibaha Mkoani Pwani Zakaria Maganga na Makamu Mwenyekiti wenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA) Mohammed Lacha na wahudhuriaji wengine mbalimbali.