
Rais wa Marekani, Donald Trump, amethibitisha kwamba rapa maarufu Diddy (Puff Daddy) amempigia simu akiomba msamaha wa rais, kufuatia hukumu ya kifungo cha miezi 50 jela.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Oval, White House, jana Jumatatu Oktoba 6, Trump alisema:
“Watu wengi wamenipigia simu wakiomba msamaha wa rais. Namwita Puff Daddy, pia yeye ameomba msamaha.”
Hii kauli inakuja huku mashabiki wa rapa huyo na vyombo vya habari vya kimataifa wakiangalia kwa karibu hatma ya msamaha huo, huku mjadala ukiendelea kuibuka kuhusu uwezekano wa Trump kutoa msamaha wa kifamilia kwa wasanii maarufu na athari zake kisiasa.
Rapa huyo, ambaye ni mmoja wa mastaa mashuhuri wa muziki wa hip hop, amekuwa akiangaziwa si tu kwa kazi zake za muziki, bali pia kwa masuala yake ya kisheria yanayovutia hisia za mashabiki na vyombo vya habari duniani.
MTOTO wa MAREHEMU MWAJABU ATOBOA MAZUNGUMZO ya MWISHO – “ALINIAMBIA MZAZI MWENZAKE AMEMPIGA”..