Picha ya pamoja viongozi wa dini na mkurugenzi wa Shirika la Ladies Joint Forum (wa kwanza kulia kwa walio kaa)
Mkurugenzi wa Shirika la Ladies Joint Forum Fransisca Mboya akizungumza kwenye mdahalo.
…………..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Shirika la Ladies Joint Forum lililoko Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kwakushirikiana na viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali wamefanya mdahalo kuhusu umuhimu wa amani kabla,wakati na baada ya uchaguzi mkuu utakao fanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Akizungumza kwenye I up mdahalo huo Mkurugenzi wa Shirika hilo, Fransisca Mboya amesema mdahalo hulo ulilenga kujifunza na kupata maoni mbalimbali yatakayoendelea kuimarisha amani katika mkoa wa mwanza na Taifa kwa ujumla.
Amesema wao kama shirika suala la uchaguzi ni la muhimu sana kwasababu linasaidia kuwapata viongozi sahihi ambao wataleta maendeleo kwa wananchi.
“Amani ni kitu muhimu sana kuanzia kwenye familia,jamii na taifa kwa ujumla hivyo kila mtu anawajibu wa kuendelea kuilinda”, Amesema Mboya.
Akichangia katika mdahalo huo mchungaji wa kanisa la EAGT Kiloleli, Jacob Mutashi alisema watu wakiepukana na migogoro, chuki, kusigana na kugombana itasaidia kuendelea kulinda amani katika nchi.
“Maneno ya uchochezi hayafai kabisa kwenye kundi la watu kwani yanaweza kuvuruga amani ya nchi yetu hivyo tunapaswa kuyaepuka”,
Kwa upande wake Ustadhi Twaha Bakari, ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza kuu la waislamu Tanzania (BAKWATA), amesema kazi Yao ni kuelimisha mema ambayo yanasaidia kulinda amani.
Awali akifungua mdahalo huo msimamizi msaidizi wa uchaguzi Jimbo la Ilemela, James Wembe alisema amani ni Tunu pekee ambayo iliachwa na Mwenyezi Mungu hivyo intakiwa kuendelea kuilinda kwa nguvu zote