
Paul Makonda, mgombea ubunge wa Arusha Mjini na aliyewahi kuwa Mwenezi wa CCM Taifa, ameitaka jamii ya Watanzania kuendelea kushirikiana kulinda amani ya Taifa, akisisitiza umuhimu wa kuondoa misingi ya ukabila na uadui kupitia mitandao ya kijamii.
Akizungumza na maelfu ya wananchi wa Sengerema, mkoani Mwanza, leo Oktoba 7, 2025, katika muendelezo wa mikutano ya kampeni za Urais kupitia CCM, Makonda alisema:
“Hatuwaguuani kwa ukabila wala udini, niwaombe sana hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania. Uchaguzi huu ni wa kikatiba, sio matatizo ya mtu wala hisia za mtu na nchi haijendeshiwi kwa matatizo, tunaendesha nchi kwa mujibu wa katiba.”
Aidha, Makonda ameeleza kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeendelea kutetea misingi ya amani, umoja, haki na kuongoza nchi kwa mujibu wa katiba, akisisitiza kuwa ushirikiano wa wananchi ni msingi wa kudumisha maendeleo endelevu na utulivu wa taifa.
“Tanzania imejengwa kwenye misingi imara ya waasisi wetu, hili na maendeleo yake umefanywa na Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,” alisema Makonda.
Makonda aliendelea kuhimiza wananchi kushirikiana, kutoenea uadui au uchochezi, na kuzingatia ushiriki wa kisiasa unaojenga amani na maendeleo.