Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Simiyu
MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amewaambia wananchi wa Jimbo la Busega Mkoani Simiyu kuwa katika miaka mitano ijayo Serikali itakwenda kujenga soko na stendi ambayo ni ahadi yake kwa wananchi hao.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika eneo la Lamadi katika Jimbo la Busega mkoani Simiyu Dk.Samia ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa Samia Suluhu Hassan akiahidi anatekeleza.
“Samia Suluhu Hassan akiahidi anatekeleza hapa Busega nilitenga fedha kwa ajili ujenzi wa soko pamoja na standı lakini mpaka leo bado mradi haujaanza kwasababu huko Halmashauri madiwani wanabishana kuhusu ujenzi wa soko liwe wapi.
“Nilitoa ahadi soko lijengwe Lamadi na Stendi ijengwe Nyashimo, hivyo tukichaguliwa tutafanya yote mawili.Nyashimo ijengwe stendi na soko lijengwe Lamadi.Hivyo madiwani amueni ingawa ahadi yangu nilishasema hapa wakati ule Stendi Nyashimo na soko Lamadi.
Katika hatua nyingine Dk.Samia amesema safari ya maendeleo huanza na moja huku akifafanua Serikali Awamu ya Sita katika Jimbo la Busanda imejitahidi kukugusa kila sekta ikiwemo katika maji, elimu, umeme,miundombinu ya barabara afya,kilimo, wafugaji,uvuvi na hakuna sekta ambayo imeachwa.
“Wananchi ni mashahidi kwa mambo yaliyofanyika katika wilaya hii,hivyo mkituchagua tutaendelea kufanya kazi katika maeno yote na Ilani inaelza yote ambayo Serikali inakwenda kutekeleza katika miaka mitano ijayo.
“Tunakwenda kujenga hospitali ya wilaya jengo la mama na mtoto, pia tunakwenda kuongeza shule za msingi na sekondari pamoja na vyuo vya VETA ili vijana wajifunze na kupata ujuzi utaowezesha vijana kuajiajiri na kuajiriwa.
“Kwenye maji Serikali imefanya kazi kubwa na sasa maji yanapatikana na kulikuwa na baadhi ya maeno miundombinu imechakaa hivyo tunakwenda kufanya matengenezo.”
Pia Dk.Samia amesema katika umeme Ilani iliyopita mwaka 2020-2025 illiekeleza tu vijiji vyote viwe na umeme kazi ambayo imefanya kwa kuwezesha vijiji vyote kupata umeme na sasa wanaendelea na vitongoji.
“Tunapeleka umeme katika vitongoji vyote kwasababu tunataka kuwa na viwanda vya kuchakata mazao hivyo lazima tuwe na umeme katika vitongoji vyote.”
Pia amesema katika barabara kazi ilishaanza na itaendelea na haitasimama lengo ni kuhakikisha barabara zinapitika mwaka mzima.