NA JOHN BUKUKJ- MUGUMU SERENGETI
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea na kampeni za Chama hicho Oktoba 10, 2025, katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, ambako amebainisha mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa uwanja wa ndege katika mji wa Mugumu.
Dkt. Samia amesema kuwa, ujenzi wa uwanja huo wa ndege upo katika Ilani ya CCM ya mwaka 2025–2030 na utatekelezwa kwa lengo la kukuza utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na maeneo jirani
Amesema hatua hiyo itawezesha watalii kutua moja kwa moja katika mji wa Mugumu, hivyo kuongeza idadi ya watalii na kuchochea fursa za ajira kwa wananchi wa eneo hilo.
Aidha, amebainisha kuwa lengo la Serikali ni kuendelea kutangaza vivutio vya utalii ili kufikia watalii milioni nane kwa mwaka ifikapo mwaka 2030, huku Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ikiwa sehemu muhimu ya kufanikisha malengo hayo.