Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope Dkt. Henry Dotto Humba tuzo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutambua mchango wake katika kusimamia ustawi wa jamii ya watu wenye ulemavu nchini, kwenye hafla iliyofanyika kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay Jijini Dar es Salaam, Oktoba 11, 2025. Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope Michael Selali
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akionesha tuzo aliyopokea kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutambua mchango wake katika kusimamia ustawi wa jamii ya watu wenye ulemavu nchini, kwenye hafla iliyofanyika kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay Jijini Dar es Salaam, Oktoba 11, 2025. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwan Kikwete, Muwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope Dkt. Henry Dotto Humba, Katibu Mkuu, Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu na Jonas Lubago, Mkurugenzi wa Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope Michael Selali. Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla ya kupokea tuzo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutambua mchango wake katika kusimamia ustawi wa jamii ya watu wenye ulemavu nchini, hafla iliyofanyika kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay Jijini Dar es Salaam, Oktoba 11, 2025. Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope.