Na.Sophia Kingimali
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema hali ya usalama katika jiji hilo inaendelea kuwa shwari, huku shughuli za kiuchumi, kijamii na kisiasa zikiendelea kwa utulivu.
Pia,Jeshi hilo linawashikilia watu wanne kwa kosa la kuendesha televisheni mtandao bila kufuata sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Octoba 15,2025 kamanda wa polisi kandaa maalim Jumanne Murilo amesema wananchi wanaendelea kushiriki katika mikutano ya vyama vya siasa, na wagombea wote wapo salama, jambo linaloonyesha hali nzuri ya amani na usalama katika kipindi hiki cha kampeni.
Jeshi hilo limeeleza kuwa linaendelea kutekeleza majukumu yake ya kila siku, yakiwemo kudhibiti vitendo vya uhalifu, na kwa ujumla hali ya jiji imeendelea kuwa tulivu. Aidha, limeongeza kuwa limeweka mikakati ya kufuatilia kwa karibu mienendo yote inayoweza kuhatarisha usalama wa wananchi.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limewakamata watu wanne kwa tuhuma za kuendesha televisheni za mtandaoni bila leseni. Waliokamatwa ni Japhet Alex Thobias
Mkazi wa Sabasaba Ukonga, Joseph Augustino Mabwe Mkazi wa
Sabasaba Ukonga wanaodaiwa kumiliki WISPOTI TV, Tegemeo
Zacharia Mwenegoha Mkazi wa Tabata Ilala mmiliki wa T.MEDIA TWO na
Elia Costantino Pius Mkazi wa Mbezi Juu Kinondoni mmiliki wa COSTA
Kamanda Mulilo ameeleza kuwa watuhumiwa hao wamehojiwa na uchunguzi wa awali umebaini kuwa wamekuwa wakifanya shughuli hizo kinyume na sheria za nchi. Polisi wamesema mara baada ya taratibu kukamilika, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
“Tunatoa wito kwa wananchi wote kuendelea kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria za nchi. Jeshi la Polisi halitasita kumkamata mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya kihalifu,” amesema kamanda Mulilo.
Jeshi hilo limewahakikishia wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuwa linaendelea kuhakikisha usalama unaimarika zaidi, huku wananchi wakihimizwa kujitokeza kupiga kura ifikapo October 29 ili kutekeleza majukumu yao ya kikatiba bila hofu, kwani polisi wapo kazini kulinda amani na utulivu.