Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi amekutana na kuzungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Mhe. Yuri Pimentel.
Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) unaofanyika Kampala, Uganda kuanzia tarehe 13 hadi 16 Oktoba 2025.
Viongozi hao wamejadili namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Venezuela hususan katika kukuza biashara, uwekezaji na utalii.
Venezuela inakamilisha taratibu zake za ndani ili kufungua Ubalozi wao nchini Tanzania.