NJOMBE, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo amemuagiza mkandarasi anayejenga Chuo kikuu huria Cha Tanzania Tawi la Njombe kuongeza Kasi ya ujenzi ili kuendana na mkataba wake unaoonesha yupo Nyuma kwa Asilimia kumi.
Agizo hilo amelitoa mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa majengo ya Chuo hicho tawi la Njombe ambapo mpaka sasa umefikia Asilimia 40 katika utekelezaji wake huku pia akionyesha kuridhishwa na ubora
Mkandarasi wa Kampuni ya Azhar Construction Company Limited Michael Mrema inayotekeleza mradi huo Unaotakiwa kukamilika Mwezi Februari Mwaka 2026 amesema atajitahidi Kukamilisha kazi kwa mujibu wa mkataba wake na kisha kuomba Serikali kumlipa Fedha anazodai.
Baadhi ya wananchi mkoani Njombe akiwemo Felix Kapugi na Mariam Kihaga Wanasema ujio wa Chuo hicho umewasaidia kupata ajira ndogondogo ambazo zinawapa ujira na kuendesha familia zao.
Kwa Upande wake katibu tawala mkoa wa Njombe Judica Omary amewataka wananchi kuchangamka Fursa ya Ujio wa Chuo kikuu kwa kuanzisha Miradi na Biashara mbalimbali.
Zaidi ya shilingi bilioni 1.08 zinatekeleza mradi huo kwa kuanza na Jengo la maabara huku changamoto za Miundimbinu ya barabara na maji ikitakiwa kushughulikiwa.