WANANCHI wa tawi la Mkoga liloko kata ya Isakalilo katika Manispaa ya Iringa wamemlilia Mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini kutatua changamoto ya mfereji wa umwagiliaji unaowasaidia wakulima wengi katika kata hiyo.
Wananchi hao walisema hayo wakati wakizungumza na mwanahabari wakati wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini Fadhili Ngajilo na kusema kuwa changamoto kubwa katika kata hiyo tawi la Mkoga ni Mfereji wa umwagiliaji na barabara ndio kubwa zaidi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wananchi hao walisema kuwa wanategemea sana kilimo katika eneo lao hivyo wamemtaka mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini Fadhili Ngajilo kuwasemea bungeni suala hilo kwani Mfereji huo ni mkombozi kwao katika kilimo.
Akijibu suala changamoto hizo, Mgombea ubunge wa jimbo la Iringa mjini Fadhili Ngajilo alisema kuwa anatambua wananchi wa kata hiyo hususani eneo la Mkoga wanakabiliana na kero kubwa mbili ambazo ni mfereji wa umwagiliaji na barabara hivyo endapo watampa ridhaa atahakikisha anapambana wapate barabara bora na atahakikisha anakaa chini na uongozi wa Halmashauri kuhakikisha wanashughulikia kerp hizo.
Alisema kuwa uwekezaji wa mradi huo wa mfereji wa umwagiliaji amewataka wananchi hao kuchangamkia fursa hiyo kwa kujikita katika kilimo cha umwagiliaji ili wawe na kilimo cha muda wote badala ya kutegemea mvua pekee na kufanya kilimo cha kisasa.
Alisema kuwa kwa kushirikiana na diwani wa kata hiyo endapo watachaguliwa watalambana kuwezesha mradi huo kujengwa kwani utawasaidia kufanya kilimo kitachowasaidia kuwa na uchumi endelevu kwa kipindi cha mwaka mzima kama vile mboga mboga na kingine badala ya kusubiri uchumi unaotokana na zao moja tu.
Ngajilo akizungumzia suala la Umeme ,maji na sekta ya afya alissema kuwa atahakikisha anapambana kutatua changamoto katika kata hiyo na kuhakikisha kwamba upande wa shule zinakuwa bora kuliko na vituo vya afya kuwa na huduma bora kwa wananchi na maji yanafika kwa wananchi wote bila kusahau suala la umeme.
Aliongeza kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha vijana wanapata kiwanja cha Mchezo kwani wamekuwa wakilalamika sana kuhusu eneo la michezo.