MAKAMU wa Rais Dkt Philip Mpango na Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ealipokelewa kwa heshima zote za kitaifa katika Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi leo asubuhi, wakati Kenya ikijiandaa kumuaga kiongozi mkongwe wa
Dkt. Mpango na Dkt. Kikwete, wamejiunga na viongozi mbalimbali kutoka mataifa ya Afrika na maeneo mengine duniani waliowasili kushiriki tukio hilo la kihistoria.
Sherehe hizo, zilizoongozwa na Rais William Ruto, zimehudhuriwa na maelfu ya waombolezaji kutoka makundi yote ya kijamii, zikionesha wazi ushawishi mkubwa aliokuwa nao marehemu Odinga katika safari ya kisiasa na ya kidemokrasia ya Kenya.
