Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kushoto),akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Zarau Wendeline Kibwe, baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika Makao Makuu ya Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambapo katika kikao hicho Benki hiyo ilisema Tanzania itanufaika na mpango mpya wa Benki ya Dunia wa kuboresha mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo katika Bara la Afrika, kupitia program yake mpya ya kuendeleza kilimo ya AgroConnect, itakayogharimu dola bilioni 9 za Marekani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (watatu kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Zarau Wendeline Kibwe (watatu kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika Makao Makuu ya Benki ya Dunia, Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambapo katika kikao hicho Benki ya Dunia ilisema Tanzania itanufaika na mpango mpya wa Benki ya Dunia wa kuboresha mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo katika Bara la Afrika, kupitia program yake mpya ya kuendeleza kilimo ya AgroConnect, itakayogharimu dola bilioni 9 za Marekani. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,WF,Washington DC, Marekani)