NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
Akizungumza na vyombo vya habari, mjane wa marehemu, Pilly Kafuye, alisema familia yao imekuwa ikiishi katika eneo hilo tangu mwaka 1977, lakini baada ya mumewe kufariki dunia, mwaka 2014 waliibuka watu wanaodai kuwa wamiliki halali wa ardhi hiyo na kuwaita wao “wavamizi.”
“Tumeishi hapa tangu enzi za mume wangu, tulilinunua eneo hili kihalali. Lakini sasa hivi tunahangaika kwa miaka yote hii bila amani. Tunaomba Rais Samia atuangalie, maana tumechoka kudhulumiwa,” alisema Bi. Kafuye kwa masikitiko.
Baadhi ya majarani wa familia hiyo walioungana kutoa ushuhuda wamesema wameitambua familia ya marehemu kama wakazi halali wa eneo hilo kwa miaka mingi, hivyo wakaiomba Serikali kufanya uchunguzi wa kina ili kuhakikisha haki inapatikana na mgogoro huo unamalizika kwa amani.



