NA DENIS MLOWE, IRINGA
TIMU. ya Kusifu na Kuabudu ya The Light ya mkoani Iringa imeandaa tamasha kubwa la kusifu na kuabudu kwa njia ya muziki linalotarajiwa kufanyika Disemba 19 mwaka huu katika ukumbi wa Sambala.
Mwimbaji na Mtumishi wa Mungu Ombeni Stony ambaye ni kiongozi mkuu wa The Light amesema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari mkoani hapa alisema kuwa lengo la tamasha hilo linalojulikana “Maskani worship gathering- Ni Shwari ni kuwaweka watu karibu na Mungu.
Stony alisema kuwa watu watakaofika katika tamasha hilo licha ya kusifu na kuabudu kwa njia ya nyimbo litakuwa na mlengo mwingine wa kuwabadilisha wamrejee Mungu na ndio maana ya maskani ni shwari ikiwa na maana kwa Mungu hakuna linaloshindikana.
Alisema kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na Matukio mbalimbali ambayo yatatokea na watu wafike kwa wingi kwa kuwa ni tamasha la bure ingawa kutakuwa na tiketi maalum kwa watu kutoa sadaka watapatiwa.
Aliongeza kuwa tamasha la Maskani litakuwa ni mwendelezo baada ya kufanya matamasha miaka ya nyuma ikiwemo maskani jogging na kila mwaka kutakuwa na matukio tofauti ya kuabudu na kusifu.
Kwa upande wake mlezi wa The Light Jesca Msambatavangu alisema kuwa tamasha hilo ni kwa ajili ya watu kumrudia Mungu kwani lina kila kitu kwa ajili yao kwani mambo mengi yataisha ila mambo ya Mungu hayataisha.
Msambatavangu alitoa wito kwa vijana ma wazee kujitokeza kwa wingi tarehe 19 mwezi wa 12 katika ukumbi wa Sambala waje kama familia ambapo kutakuwa na kifurushi cha familia, watu wawili nk hivyo wanakaribishwa.
Alisema kuwa kubwa zaidi ni kumwamudu na kumsifu Mungu kwa wale waliokata tamaa ya kuoa au kuolewa waje kupata faraja na mafunzo katika tamasha hilo.
“Vijana wanakaribishwa ukutane na Mungu aliyekuumba Kila mara ufike katika matamasha ya dini kuliko kule ambapo wengi wanapenda kwenda kwenye mabar nk tutaendelea kuwasaidia katika sualaa la Kusifu na kuabudu ” alisema.
Naye Amenye Kalinga mkuu wa kitengo cha Mawasiliano katika Timu ya the Light alisema kuwa tamasha hilo kutakuwa na wasanii mbalimbali wakiongozwa na Clement Paul, Donick Mwakatobe, na mtumishi mwenyeji Ombeni Stony na Vctor Maestro.