Mganga mkuu wa mkoa ,Dokta Charles Mkombachepa akizungumza kwenye bonanza hilo jijini Arusha leo.
Katibu wa bodaboda wilaya ya Arusha, Richard Magembe akizungumza kwenye bonanza hilo jijini Arusha.
………..
Happy Lazaro, Arusha .
Vijana wametakiwa kushikiri kikamilifu katika kufanya mazoezi kwa ajili ya usalama wa afya zao pamoja kuondokana na magonjwa yasiyoambukizwa.
Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Mganga mkuu wa mkoa ,Dokta Charles Mkombachepa wakati akizungumza kwenye bonanza la afya na michezo lililoandaliwa na Arusha jogging club likiwa na malengo pia ya kuhamasisha uchaguzi wa oktoba 29 mwaka huu , lililofanyika katika uwanja wa Ngarenaro jijini Arusha.
Amesema kuwa ,bonanza hilo limeshirikisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondari za jiji ambapo waliweza kucheza michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa mikono,kukimbia ambapo washindi waliweza kupatiwa medali mbalimbali pamoja na kombe.
“Tumekuwa tukihamasisha watu kufanya mazoezi kwani yanasaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia magonjwa yasiyoambukizwa ikiwemo sukari na afya ya akili ambapo kwa kufanya mazoea kunasaidia hata kuondokana na gharama za kwenda kutibiwa magonjwa ambayo yangeweza kuzuiwa kwa kufanya mazoezi .”amesema dokta.
“Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amepambana na kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya nchini ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi kwa ajili ya usalama wa afya zao na kujikinga na magonjwa mbalimbali.”amesema dokta.
“Napenda kutoa wito kwa vijana pamoja na wananchi kwa ujumla kushiriki na kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura oktoba 29 kwa ajili ya kuwachagua viongozi wazuri wenye uchungu na nchi yao kwani ni wajibu wa kila mmoja kutimiza haki yake ya msingi ya kupiga kura “amesema Dokta.
Ameongeza kuwa, bonanza hilo ni endelevu lengo likiwa ni kuhamasisha watu kufanya mazoezi kwa faida za afya yao na kuepukana na magonjwa mbalimbali kwani kwa kufanya mazoezi kunaweza kupunguza gharama kubwa za matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza ambayo yanaweza kuzuiwa kwa kufanya mazoea kwani mazoezi ni kinga kubwa mwilini.
“Mtu.yoyote anapotaka kufanya mazoezi sio lazima aende uwanjani mazoezi yanaweza kufanyiwa mahali popote hata nyumbani kwako , natoa wito kwa mashirika pamoja na halmashauri kutekeleza maagizo ya serikali kwa kufanya mazoezi mara kwa mara kwa ajili ya kulinda afya zao na kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.”amesema.
Naye Katibu wa bodaboda wilaya ya Arusha, Richard Magembe amesema kuwa,bonanza hilo limekuwa chachu kubwa kwa vijana pamoja na wanafunzi hao kwani linawahamasisha wao kufanya mazoezi mara kwa mara kwa ajili ya kulinda afya zao huku akiwataka vijana kuhakikisha wanashiriki kwa wingi kwenye zoezi la kupiga kura oktoba 29 mwaka huu.
Naye Mwalimu wa Arusha sekondari, Honoratha Bitumbilo amesema kuwa, kupitia bonanza hilo wanafunzi wameweza kushiriki kikamilifu katika kufanya mazoezi kwani mazoezi ni afya huku akiwataka vijana kuwa mstari wa mbele kuhamasisha michezo.
Naye Mmoja wa vijana Grace Tarimo amewataka vijana kujitokeza kwa wingi kufanya mazoezi kwa ajili ya afya zao huku akitoa wito kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi oktoba 29 kwenda kujiandikisha.