Na Said Mwishehe
ALIYEKUWA Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ezekia Wenje ameendelea kutoa siri za Chama hicho ambapo amesisitiza wao wenyewe ndio wameamua wasishiriki Uchaguzi mkuu mwaka huu.
Aidha amesema yeye amekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu kwa miaka 15 na hajawahi kutoka,hivyo anapowaambia watu wanaumwa huko CHADEMA halafu wewe unabisha kwani ulikuwepo.
Wenje ameyasema hayo leo Oktoba 18,2025 mbele ya maelfu ya wananchi wa Mji wa Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa wakati wa mkutano wa kampeni za Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
“Wanasema nchini kwetu kwa sasa demokrasia inaminywa .Nataka kuuliza demokrasia ni nini na demokrasia inayokuwa ni ipi? Baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 nilikimbia nchi, Godbless Lema naye akakimbia, Tundu Lissu ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha wakunja ngumu naye alikimbia.
“Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alipoingia akaja na maridhiano tuliokuwa tumekimbia nchi tumerudi nchini.Sasa demokrasia ni nini?
“Tulikuwa na kesi 417 ziliondolewa baada ya maridhiano, kama Samia yote amefanya demokrasia nini? Aliruhusu mikutano ya hadhara lakini aliruhusu na katika mikutano tukawa tunatukana.”
Wenje ambaye kwa sasa amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa CHADEMA pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Kandq ya Ziwa ambayo inajumuisha mikoa mitatu ya Mwanza,Kagera nq Geita na tangu amejiunga na CCM amekuwa Akieleza ukweli kuhusu yaliyokuwa yanaendelea katika Chama chake cha zamanı.
“Baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 tuligoma kuchukua ruzuku lakini tulimwambia Mwenyekiti Wetu akazungumze na Rais Dk.Samia aliruhusu tukapewa ile ruzuku.
“Nikiwa kule nilikuwa Mwenyekiti wa kamati ya fedha na kwamba baada ya ruzuku ndio tukapata na ofisi ya Chama pale Mikocheni,mimi ndio nilinunua.
“Nchi gani watu wanatukana viongozi usiku kucha na hawakamatwi.Nimekuwa katika kampeni hii tangu nilipojiunga CCM na kote ambako tumepita unaona mabilioni ya fedha yaliyotumika kufanya maendeleo.Ukiangalia shule,barabara,afya, kilimo,maji na huduma muhimu kazi kubwa imefanyika.Namba hazidanganyi.”
“Ndugu zangu ile SGR inapandwa na CCM peke yake? Acheni porojo ,acheni mikwara njooni na hoja za kupambana na CCM. Nimekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu kwa miaka 15 sijawahi kutoka,nakwambia watu wanaumwa huko wewe unabisha,ulikuwepo?
“CHADEMA hatujazuiwa kufanya uchaguzi bali tulikataa wenyewe,tulienda mkutano mkuu tukasema hatutashiriki.Hakuna aliyezuia tusiende kusaini ,sababu zipo na naweka akiba nitazisema siku nyingine.”
Akiendelea kuzungumza Wenje amesema kwamba Mwenyekiti wa wakunja ngumi amekuwa mbunge mara mbili kwa Tume ile ile ya Uchaguzi.
“Na hapa Nkasi alikuwepo Mbunge wa CHADEMA dada Aida Kenani .Ukweli wamekuwa waoga ,wameweka mpira kwapani.Otkoba 29 ni siku muhimu ya demokrasia ya Tanzania hivyo twendeni tukaiambie dunia demokrasia iko Tanzania