
Klabu ya Young Africans SC imeanza hatua ya pili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League 2025/26) kwa kipigo cha bao 1-0 dhidi ya wenyeji Silver Strikers ya Malawi.
Mchezo huo wa mkondo wa kwanza umepigwa katika Uwanja wa Taifa wa Bingu, jijini Lilongwe, ambapo bao pekee la mchezo lilifungwa dakika ya 76 na Andrew Joseph akiitendea haki timu yake ya nyumbani.
Kipigo hicho kinaiweka Yanga kwenye nafasi ya kusaka ushindi wa lazima katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Oktoba 25, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, ili kutinga hatua ya makundi ya CAFCL msimu huu.
FT: Silver Strikers 1–0
Yanga SC
76’ Andrew Joseph
Â