
Timu ya vijana ya chini ya miaka 20 ya Morocco iliandika historia Jumapili baada ya kushinda taji lake la kwanza la Kombe la Dunia kwa vijana wa chini ya miaka 20 “FIFA U-20 World Cup” kwa kuifunga Argentina mabao 2–0 kwenye fainali.
Shujaa wa mchezo alikuwa mshambuliaji Yassir Zabiri, aliyefunga mabao yote mawili katika dakika ya 12 na 29, na kuwasaidia Morocco kuwa taifa la kwanza kutoka Afrika kushinda taji hili tangu ishinde Ghana mwaka 2009.
Argentina, ambayo haikupoteza mchezo wowote kabla ya fainali, ilikuwa ikitafuta taji la saba lakini ilikosa wachezaji wake wawili muhimu Claudio Echeverri kutoka Bayer 04 Leverkusen na Franco Mastantuono kutoka Real Madrid CF.
Safari ya Morocco kuelekea ubingwa ilikuwa ya kuvutia walimaliza kileleni baada ya kuwashinda Uhispania, Brazil na Mexico Kbaada yakuvuka makundi walizitoa Korea Kusini, Marekani na Ufaransa kufika fainali.