Na Mwandishi Wetu
Kamati iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila imekamilisha ripoti na kumkabidhi Mjane Alice Haule kuwa msimamizi wa mirathi ya watoto wa Wanne Alice akiwa na Watoto wawili wa Marehemu Mme wake.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kuwa wakati anashughulikia mgogoro huo kati ya Alice Haule na Mfanyabiashara Mohamed Yusuf Ally wote waliitwa lakini Mfanyabiashara huyo hakuweza kufika kwa kusema anaumwa yuko nchini Afrika Kusini ambapo ametoa tena siku tano na asipokwenda atafuatwa huko huko kuja nchini kwa vyombo vya vya Serikali.
Amesema kuwa Kamati hiyo ilibaini kuwa marehemu walikopeshana na mfanyabiashara huyo lakini Mke wake hakuhusika na kufanyika kwa baadhi ya nyaraka za kughushi za Mke wa Marehemu ikiwemo saini.
Amesema kuwa Serikali kamati iliyoundwa ingekuwa ya kula rushwa haki hiyo isingepatikana lakini imeonyesha weledi hadi kufikia kupewa hati ya usimamizi wa mirathi kwa Alice Haule.
Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa ulinzi uendelee pasipo kubugudhiwa na mtu yetote na akitokea kufanya hivyo asisite kuwasiliana na vyombo hata usiku wa manane.
Hata hivyo amesema kuwa Mfanyabiashara huyo analitumia jina la Familia ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan vibaya na kutaka kuacha mara moja na hakuna uhusiano kwa vitu anavyovifanya.
Hata hivvyo Mkuu wa Mkoa amemkabidhi sh.milioni 10 kwa ajili ya kufanya baadhi matengenezo ya nyumba baada kuharubiwa na mabausa waliokwenda kuwahamisha familia ya Alice Haule.
Mkuu Mkoa amesema kuwa kuteuliwa kwao ni kuna umuhimu katika kushughulikia masuala ya wanyonge na kama wangekuwa wala rushwa haki hiyo Alicena familia yake ingekuwa imepotea.
RC Chalamila ametaka wananchi kujitokeza katika dhulma hizo ili haki zao zipatikane kwa serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan iko kwa ajili ya wananchi wake.
Naye Alice Haule amesema kuwa anaishukuru Serikali na Mkuu wa Mkoa kupata haki yake aliyoipigania kwa muda mrefu .