
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili na kupokelewa kwa shangwe na maelfu ya wananchi, viongozi wa dini, machifu, wazee na viongozi wa CCM katika viwanja vya Kecha, wilayani Ilala, Jijini Dar es Salaam, leo.
Dkt. Samia anaendelea na mikutano yake ya kampeni ndani ya mkoa wa Dar es Salaam, aliyoianza jana Oktoba 21 katika wilaya za Kinondoni na Ubungo, akinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2025/30), sera na ahadi zake kwa wananchi. Pia amewaomba wananchi kupiga kura za Ndiyo kwa mafiga yote matatu katika uchaguzi ujao.
Mikutano hii imejumuisha viongozi wa chama, jumuiya zake, viongozi wa dini, machifu na wazee, huku wananchi wakionyesha shauku na kushiriki kwa wingi katika kupokea mgombea huyo wa urais.