…………….
NA DENIS MLOWE, IRINGA
MKUU wa Mkoa wa Iringa, Kheri James amekabidhi magari nane kwa jeshi la polisi mkoani hapa na gari jingine litakuja baadaye kutimiza idadi ya gari 9 ambayo yatasaidia kuongeza ufanisi kwenye utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Katika magari hayo ya kisasa , moja la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi na magari mengine kwa ajili ya vitengo mbalimbali ndani ya jeshi ikiwemo moja kwa ajili ya maofisa upelelezi wa jeshi mkoani hapa.
Akizungumza mara baada ya zoezi la kukabidhi magari hayo, RC James alisema magari hayo yametolewa na serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ili kutatua changamoto ya vitendea kazi ambavyo vilikuwa vinalikabili jeshi hilo hivyo kusaidia katika majukumu yake ya kila siku.
Rc. James alisema kuwa jeshi la polisi limekuwa la mfano katika utendaji kazi wake hivyo magari hayo yataongeza umakini na kuhakikisha kwamba kuwalinda raia na mali zao ni la uhakika.
Alisema kuwa kutokana na utendaji kazi wa jeshi la polisi limejionyesha kutokana na wananchi kuendelela kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo hivyo muhimu kuendelea kuwapa ushirikiano wananchi.
Aidha alimpongeza Mkuu wa Jeshi la polisi Tanzania IGP Wambura kwa kuleta mageuzi makubwa katika jeshi la polisi na kuwapatia kamanda SACP Allan Bukumbi kutokana na utendaji kazi katika mkoa wa Iringa.
Rc Kheri James alisema kuwa ajenda ya usalama ni ajenda kubwa na kutokana na kuwa na ufanisi mkubwa limeongeza eneo la ajira kwa vijana kujiunga na jeshi la polisi ili kuongeza utendaji kazi.
Vile vile alisema kuwa jeshi hilo limeongeza Hali na stahiki za askari na kuuwekeza kwenye vitendea kazi nq kuimarisha mafunzo kwa askari ambayo yanafanya jeshi kuwa la mfano ndani na nje ya nchi.
Aidha aliwashukuru Baadhi ya wadau ambao wamekuwa wakijenga vituo vya polisi haya ni mageuzi makubwa na lazima jamii ifahamu jeshi hili ni letu kwa maslahi ya wananchi.
Aidha alitoa wito kwa halmashauri Kutenga maeneo ya kujenga vituo vya jeshi la polisi na halmashauri zisiogope kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi.
Alitoa ushauri kwa jeshi la polisi kuwa magari hayo ni imara na yanahitaji matunzo na yamepokelewa katika hali bora na yatumike kwa kazi za jeshi polisi na si vinginevyo.