Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MRATIBU wa Uchaguzi Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam Marry Chatanda amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imetekeleza vyema ilani ya uchaguzi ya CCM (2020 – 2025) katika sekta mbalimbali nchini.
Aidha amesema katika kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu utakaofanyika Oktoba 29,2025 wameshirikia na viongozi wa chama mkoa huo katika kuhakikisha ushindi kwa CCM.
Akizungumza leo Oktoba 23,2025 mkoani Dar es Salaam mbele ya Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, Chatanda amesema pia wanawake wamejipanga vema kuhakikisha Dk.Samia anashinda kwa kishindo.
Chatanda ambaye pia Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) amesema kuwa kupitia kamati mbalimbali ambapo zaidi ya milioni 15 wamefikiwa na lengo la kamati hizo ni kuwafikia wanawake zaidi ya milioni 16 kwani kundi hilo ndilo linaloongozwa kwa mwitikio mkubwa kujitokeza kupigakura.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu, ametumia mkutano huo ambao Mgombea Urais Dk.Samia anahitimisha kampeni zake kwa mkoa huo amewasilisha salamu za Wazee wa Dar es Salaam ambapo wamesema kelele za mitandaoni ni za watu waliokosa staha.
Kwa upande wake Mgombea Ubunge Jimbo la Iramba na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema Dk. Samia katika miaka
Minne na nusu ya uongozi wake amejenga shule za msingi zaidi ya 2,700 na shule za sekondari zaidi ya 1,000.
Pia amesema kuwa kwa kwanza Tanzania imeingia katika historia kwa ya kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji kwa kutumia fedha za ndani.
Kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu, amesema Tanzania imetumia fedha zake za ndani kugharamia uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba 29.
“Tumetimiza ndoto ya Mwalimu Nyerere ya kujitegemea. Leo hii tuna fedha hadi za kujenga reli mpaka Mwanza, tunasubiri mkandarasi aliwasilishe hatia zake za malipo tu.”
Wakati huo huo aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Victoria, Ezekia Wenje, amesema kwa sasa ndio mwisho wa chama hicho kwa sababu kimewahadaa Watanzania kwa muda mrefu.
Aidha amesema CHADEMA kususia uchaguzi siyo suluhisho la utatuzi wa changamoto bali jambo sahihi ni kufanya mazungumzo.
“Mtu anaamka asubuhi yupo Marekani kazi yake kuleta propaganda kulisha watu uongo. Nchii hii ni kubwa kuliko mtu, kura tutapiga na nchi itasonga mbele.”
Mwisho