Mshindi wa Mashindano ya @missuniversetanzania mwaka 2025 mwanadada @naisae.yona, amekabidhiwa rasmi gari jipya aina ya Hyundai kutoka kwa @hyundai_tanzania lenye thamani ya shilingi milioni 49.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo Oktoba 22, 2025 ambapo @naisae.yona ametajwa kuwa si mrembo tu, bali ni kielelezo cha kizazi kipya cha wanawake wa Kitanzania wenye nidhamu, maono, ujasiri na moyo wa kujitolea kwa jamii.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Millen Prive Co. & Lifestyle na Muandaaji wa Miss Universe Tanzania, Millen Magese amesema;
“@naisae.yona si mrembo tu, ni kioo cha kizazi kipya cha wanawake wa Kitanzania wenye maono, nidhamu na ujasiri, wenye mioyo mikubwa ya kutoa na kusaidia jamii, kupitia ushindi wake tunaiona sura mpya ya Tanzania inayokwenda kuwa kioo cha urembo duniani.”
Kwa upande wake, @naisae.yona amesema leo ni siku yenye maana kubwa kwake, akieleza kuwa amefanikiwa kutimiza ndoto yake kubwa maishani na kwamba ataendelea kuwa mfano na sauti ya kuhamasisha wanawake na wasichana kuamini katika ndoto zao.
Miss Universe Tanzania, Naisae Yona ataondoka nchini Jumatatu ya October 27,2025 kuelekea nchini Thailand yatakapofanyika mashindano ya Miss Universe.
Aidha @hyundai_tanzania wameahidi kutoa magari ya msafara utakaomsindikiza Naisae Airport wakati akiondoka nchini.