Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Zanzibar
MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ametaja mambo muhimu ambayo Serikali zote mbili zitakwenda kuyasimamia kwa nguvu zote ikiwemo kuulinda Muungano ambao umekuwa na faida kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Akizungumza leo Oktoba 24,2025 mbele ya maelfu ya wananchi wa Zanzibar alipokuwa akihitimisha kampeni zake za uchaguzi mkuu kwa upande wa muungano Dk.Samia ametumia nafasi hiyo kueleza masuala mbalimbali ambayo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanzibar watayapa mkazo zaidi.
“Serikali za Chama Cha Mapinduzi kwa maana ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni watekelezaji wa ahadi zinazotolewa na Chama Cha Mapinduzi.
“Tukifanya tathimini ya utekelezaji wa Ilani ya 2020-2025 kazi kubwa imefanyika na kwa upande wa Ilani ya 2025-2030 mambo mengi yanakwenda kufanya na makubwa zaidi niwahakikishie mkitupa ridhaa tutaendelea kushirikiana kwa karibu kufanikisha yale yote yaliyoagizwa na Ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi
“Nitumie fursa hii kugusia machahe kwanza Muungano wetu, niwahakikishie tunakwenda kuulinda kwa nguvu zote kwani ni muungano wenye faida kwa pande zote ,muungano huu unafaida kwa Zanzibar,kwa Bara tunategemeana ,hivyo tunakwenda kuuulinda kwa nguvu zote.
“Jambo la pili tunakwenda kulifanyia kazi kwa nguvu zote ni maendeleo jumuishi maendeleo yanayomchukua kila Mtanzania kwenda naye .Na katika eneo hili tutakwenda kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha huduma za jamii kama chakula,maji ,elimu ,afya na umeme unamfikia kila mtu
“Natambua kwasasa tunachangamoto ya umeme hapa Zanzibar lakini nataka niwahakikishie mimi na Dk.Hussein Ali Mwinyi tumesimama imara kumaliza kadhia hii,si muda mrefu Zanzibar itakuwa na umeme wa uhakika saa 24 kwa wiki yote.”
Akieleza zaidi Dk.Samia amesema jambo jingine.ambalo wanakwenda kulisimamia ni uwezeshaji wananchi kiuchumi,mitaji na fursa za ajira,kuajiriwa na fursa za kufanyabiashara.
Amesema huko nako Serikali hizo zinakwenda kuweka mguvu kubwa ili waweze kuhakikisha vijana wanapata ajira au kuajiri na kubwa waweze kuendesha maisha yao.
Mgombea urais Dk.Samia pia amesema Serikali hizo zinakwenda kuongeza nguvu kusimamia ni kukuza uchumi mkubwa kwa pande zetu mbili za muungano na kwba wanafanyakazi kwa pamoja kukuza uchumi wa nchi.
“Tumefanya kazikubwa kuhakikisha vichocheo vya uchumi huu tumeviimarisha.Vichocheo hivi ni usafiri na usafirishaji watu na bidhaa zote kwa njia zote za majini, barabara na anga ,kote tumehakikisha tunaimarisha na tutaendelea kwani tukirahisha usafiri tunarahisisha biashara na tunarahisha shughuli za watu wetu.
“Lakini suala jingine la vichocheo vya uchumi mkubwa ni nishati.Pia tunakwenda kufanyia kazi kwa pamoja sekta za uzalishaji na kwa hapa Zanzibar sekta hizo ni za uchumi wa bluu, utalii na kilimo ambapo tunakwenda kuvalia chuga tuhakikishe tunafanya vizuri.”
Pia amesema kwa sekta ya utalii kwa Tanzania bara lengo ni kufikia watalii milioni nane wa ndani na nje ya nchi na kwa Zanzibar lengo lao ni kufikia watalii milioni moja lakini wao wanahesabu watalii wa nje peke yao.
“Hawajaweka wa Bara wanaokuja kutembea wanachukulia ni Watanzania lakini kule Bara ukitoka kwenda hifadhi ya Mikumi unahesabika kama mtalii na tunakuweka kwenye hesabu.Kwahiyo hizo ndio sekta ambazo tunakwenda kuzifanyia kazi ili tujenge uchumi mkubwa.”
Akizungumza uchumi mkubwa amesema Serikali hizo zimefanya vizuri sana huku akifafanua baada ya changamoto za COVID-19 uchumi ulianguka mpaka asilimia nne lakini kwa Zanzibar wao uchumi wao mwaka huu umefikia mko asilimia saba.
“Kwa upande upande wa bara tuko asilimia 6 na tunatarajia mwakani tutarudi kwenye asilimia saba.Kwenye uchumi wa bluu kule kuna mafuta na gesi lakini uvuvi wa bahari kuu huko kunatoa kwa ajira za vijana wetu.”
Kwa upande wa utalawa bora amesema Ilani ya Uchaguzi Mkuu imeahidi Katiba mpya katika kipindi cha miaka mitano ijayo.”Wenzetu vyama vya upinzani wamekuwa wakipigia kelele muda mrefu lakini hata waliomo CCM nao baadhi yao wamekuwa wakilisemea suala hilo.
“Tumesema miaka mitano ijayo tunakwenda kujenga mazingira bora,mazingira ya utawala bora , mazingira ya utawala wa sheria, tunakwenda kuwa na Katiba mpya .Hiyo ndio Ilani yetu inavyosema.”
Kuhusu ulinzi na usalama wa nchi na raia zale Dk.Samia amesema hakuna tatizo kwani Serikali zote mbili zimeweza kuipeleka nchi vizuri na hakuna lolongo kwenye hilo ,lakini ameahidi kuendelea kulisimamia vema.
Akizungumza diplomasia amesema ni suala ambalo halina mbadala hivyo wanakwenda kulisimamia vema ili kuendelea kuiweka nchi vizuri ,iendelee kuaminika na kutegemewa.
“Tunafanya hayo ili tukilinda utu heshima na utaifa wetu kwani hatujipeleki huko tukaweka rehani uhuru wetu, mapinduzi yetu au heshima yetu hapana, tunakwenda huku tukilinda heshima ya taifa letu.






.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)



