

Leo amezaliwa nyota hatari zaidi kuwahi kutokea katika kikosi Cha Manchester United na timu ya taifa ya England WAYNE MARK ROONEY!
Wayne Mark Rooney alizaliwa tarehe 24 Oktoba 1985 mjini Croxteth, Liverpool, Uingereza. Akiwa mtoto, alianza kuonyesha kipaji cha ajabu cha kucheza soka katika mitaa ya eneo lake na baadaye akaingia kwenye akademi ya Everton akiwa na umri wa miaka tisa.
Uhodari wake ulionekana mapema, na akiwa na umri wa miaka 16 tu alicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya England mwaka 2002 na kufunga bao maarufu dhidi ya Arsenal. Uchezaji wake wa nguvu, akili ya mchezo, na uwezo wa kufunga mabao ulifanya Rooney kuwa mmoja wa wachezaji wachanga waliovuma haraka zaidi nchini Uingereza, na hivi karibuni alijiunga na Manchester United, ambako taaluma yake ilianza kupaa rasmi.
Takwimu za Rooney
759 Games
120 Caps
366 Goals
189 Assists
Idadi ya makombe ambayo nyota huyu amewahi kushinda
Premier League: 5
League Cup: 4
FA Cup: 1
Champions League: 1
Europa League: 1
Club World Cup: 1
Mfungaji Bora wa muda wote wa Man United
Wayne Rooney ametimiza miaka 40 , Je? unakumbuka tukio gani kutoka kwa Rooney ?
Imeandikwa @mohusein_15









