Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Kamati Maalum ya Uangalizi ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu Mageuzi ya Taasisi za Umoja wa Afrika, uliyofanyika kwa njia ya mtandao akiwa Jijini Dodoma.
Mkutano huo, umeongozwa na kinara wa mageuzi ya taasisi za Umoja wa Afrika ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na wawakilishi wa kisekta wa Umoja wa Afrika.










