KATIKA kuendeleza jitihada zake za kuchangia maendeleo ya michezo nchini, kampuni ya michezo ya kubashiri mtandaoni, Meridianbet, imeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kusaidia jamii kupitia shughuli za kijamii (CSR), kwa kugawa vifaa vya michezo kwa kikundi cha Amani Jogging kilichopo Vingunguti, Jijini Dar es Salaam.
Kupitia mradi huu wa kijamii, Meridianbet ilikabidhi jezi na mipira ya kisasa ya michezo kwa wanachama wa Amani Jogging, kama sehemu ya kusaidia juhudi za vijana na watu wazima wanaojituma kudumisha afya, umoja na maendeleo ya michezo katika jamii.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, mwakilishi wa Meridianbet alisema:
“Tunatambua umuhimu wa michezo katika kuleta afya, umoja na kuimarisha mahusiano ya kijamii. Ndiyo maana Meridianbet imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia vikundi vya michezo vya jamii, ili kuhakikisha kila kijana na mwanajamii ana nafasi ya kushiriki kwenye shughuli za michezo kwa urahisi zaidi. Tunahamasisha vijana wote kuendelea kutumia muda wao vizuri katika michezo na kujiepusha na vitendo visivyo na tija.”
Jisajili na Meridianbet na cheza michezo ya kasino ya mtandaoni ili kupata ushindi kirahisi zaidi. Pia, ongeza maokoto yako kwa kubashiri michezo yenye ODDS KUBWA ZAIDI!. PIGA *149*10# au tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz
Kwa upande wake, kiongozi wa Amani Jogging, alishukuru kampuni ya Meridianbet kwa moyo wa upendo na kujali jamii, akisema kuwa msaada huo umekuja kwa wakati muafaka:
“Tunaishukuru sana Meridianbet kwa kutuona sisi wana Vingunguti. Vifaa hivi vitatusaidia sana kuendelea na mazoezi yetu kwa ari zaidi. Ni nadra kupata wadau wanaotambua juhudi za vikundi vya michezo vya jamii kama sisi, na kwa hili tunasema asanteni sana.”
Meridianbet imekuwa ikijipambanua si tu kama kampuni ya michezo ya kubashiri, bali kama mshirika wa maendeleo ya jamii, ikitekeleza miradi mbalimbali ya kijamii katika sekta za afya, elimu, michezo, na mazingira. Hii ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa Meridianbet kuhakikisha jamii inanufaika moja kwa moja na mafanikio ya kampuni.
Kwa upande wa michezo, Meridianbet imekuwa ikifanya mashirikiano na vikundi mbalimbali nchini, ikiwemo timu za vijana, mashindano ya mitaani, na makundi ya jogging kama Amani Jogging, ili kuhamasisha mazoezi ya mwili, kuimarisha afya, na kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kukuza michezo nchini.
Kupitia kaulimbiu yake, “Meridianbet – Tunacheza Pamoja na Jamii”, kampuni inaendelea kuthibitisha kuwa michezo sio burudani pekee, bali ni chombo cha kuleta mabadiliko chanya katika jamii.









