Waziri mstaafu wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu.
……….
Na Hellen Mtereko, Mwanza.
Zikiwa zimesalia siku tano kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofayika Oktoba 29, 2025 Waziri mstaafu wa Maliasili na Utalii amewasili jijini Mwanza kwajili ya kuzungumza na makundi ya vijana juu ya umuhimu wa kuilinda amani ya nchi.
Nyalandu amewasili Mwanza leo Oktoba 24, 2025 ambapo amesema yupo hapa kwaajili ya kuzungumza na nguvu kazi ya Taifa (VIJANA) sanjari na kuwasisitiza kupiga kura.
Amesema vijana wanapopiga kura inakuwa vizuri sana kwani wanaenda kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo.
“Nawasihi sana vijana pamoja na kupiga kura jitahidini kuilinda na kuitunza amani ya nchi yetu kwani ni Tunu tuliyopewa na Mungu”, amesema Nyalandu.
Aidha, ameeleza kuwa kila mtanzania anawajibu wa kuilinda amani hivyo siku ya kupiga kura wajitokeze kwawingi kwaajili ya kutekeleza zoezi hilo la kikatiba.







