

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amekabidhi kiasi cha shilingi milioni tano (5,000,000/=) kwa timu ya Umoja wa Maveterani wa Soka Tanzania (UMSOTA) kama zawadi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amekabidhi fedha hizo Oktoba 23, 2025 jijini Dar es Salaam, katika hafla maalum ya kuipongeza timu hiyo baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya soka ya Maveterani Afrika Mashariki, yaliyofanyika tarehe 1 Oktoba 2025 nchini Kenya.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UMSOTA Paul Ambrose Lusozi maarufu kama Father aliishukuru Serikali kwa kutambua mafanikio yao, akiahidi kuwa timu hiyo itaendelea kushiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuimarisha umoja na kukuza michezo miongoni mwa maveterani.
Mashindano hayo ya Afrika Mashariki yalihusisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.

VIONGOZI wa DINI NYANDA za JUU KUSINI WATAKA VIONGOZI wa SIASA KUDUMISHA AMANI…









