*Ujenzi wa madarasa mpya na maboresho ya miundombinu ya usafi yatasaidia zaidi ya wanafunzi 1,000
Babati
SERIKALI ya Japani kupitia mpango wake wa ruzuku unaojulikana kama Grant Assistance for Grassroots Human Security Projects (GGHSP) imejitolea kutoa hadi Dola za Marekani 109,203 (takriban TSh 275 milioni) kusaidia ujenzi wa nyumba ya madarasa pamoja na maboresho ya mazingira ya usafi katika Orng’adida Primary School iliyopo wilayani Babati, mkoani Manyara.
Mradi huo umeidhinishwa rasmi Oktoba 22, 2025 ambapo mkataba ulisainiwa na Balozi wa Japani nchini Tanzania, Mikami Yoichi, na Ms Roselyne Mariki, Meneja wa nchi wa shirika So They Can Tanzania.










