Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Zanzibar
ALIYEKUWA Mjumbe wa Kamati Kuu kwa miaka 15 na Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Ziwa Victoria Ezekia Wenje metoboa siri ya Chama hicho kushindwa kushiriki uchaguzi mkuu mwaka huu ni kutokana na kukosa maandalizi pamoja na ukata wa fedha.
Wenje ambaye kwa sasa amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametoa siri hiyo leo Oktoba 24,2025 alipokuwa akizungumza katika mkutano wa kampeni za mgombea urais kupitia Chama hicho Dk,Samia Suluhu Hassan ambaye amehitimisha kampeni zake kimuungano katika Visiwa vya Zanzibar.
“Iko hvi sisi tulikaa tukaangalia hali hivyo,hatukuwa na maandalizi, hatukuwa a fedha na mgombea wetu hakuwa hata na uwezo wa kuwa na fedha Sh. milioni 100.Baada ya kuona hatuna maandalizi ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu ndio tukaja na no reform no election
“Tulikataa wenyewe CHADEMA kwa kuwa hatuna maandalizi ,tulikaa kikao cha kamati kuu na tukaamua tusishiriki uchaguzi mkuu.Ndio maana hata tulipoandikiwa barua na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ya kwenda kusaini fomu ya maadili ya Uchaguzi hatukwenda saini.
“Nataka niwape stori ya upande wa pili walikubaliana wenyewe wasiende hivyo hakuna mtu aliyewazuia kushiriki.Serikali haijawazuia kushiriki uchaguzi huu.”
Aidha amesema hakuna Chama cha siasa ambacho kimekimbia uchaguzi halafu kikabi kuwa salama,hakipo.
Wakati huo huo Wenje amesema Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani aliamua kuja na maridhia ambayo yamewezesha kesi 417 kati ya kesi 419 ambazo zilikuwa zinawakabili wafuasi na wanachama wa CHADEMA kufutwa.
“Tulikuwa na kesi 417 zilifutwa kati ya kesi 419,Mwenyekiti CHADEMA alikiri kesi zake saba zilifutwa,kama hiyo sio demorasia ni nini?Tuliokimbia nchi Rais Dk.Samia ulituruhusu turudi sasa demorasia ni nini? Ndio maana nimekuja kueleza stori ya upande wa pili.
“Tulitaka wakurugenzi wa halmashauri wasimamie kura, leo hii hawashiriki, tulitaka, mtu anayegombea peke yake asipite bila kupingwa na leo hii sheria imeweka wazi lazima mgombea apigiwe kura.”
Aidha Wenje amesema kuwa yeye ndio alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya fedha,alifika Zanzibar kuangalia jengo la ofisi lakini aliporudi Dar es Salaam CHADEMA kwasababu ya kiburi.
“Wanaidharau Zanzibar kwamba haina nguvu lakini chama ambacho kinaheshimu Tanzania Bara na Zanzibar ni Chama Cha Mapinduzi.
“Wakati Rais Dk.Samia anakuja na mpango wa kuiboresha bandari ya Dar es Salaam CHADEMA walisema kuwa anauza bandari kwasababu Rais anatokea Zanzibar lakini leo hii bandari ya Dar es Salaam imekuwa kimbilio la watu mbalimbali.”















