

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Afrika (AUEOM), ulioongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Botswana, Mokgweetsi Masisi, ambaye pia ni Kiongozi wa Misheni hiyo.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar, ambapo viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu uimarishaji wa demokrasia, amani, na ushirikiano wa kikanda katika Bara la Afrika.
Rais Samia amepongeza Umoja wa Afrika kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za nchi wanachama katika kuhakikisha chaguzi zinakuwa huru, za haki na zenye amani. Aidha, amesisitiza dhamira ya Tanzania kuendeleza misingi ya utawala bora, uwajibikaji, na mshikamano wa kijamii.
Kwa upande wake, Masisi ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa usalama na ushirikiano mzuri walioupata wajumbe wa AUEOM wakati wa majukumu yao nchini, na amepongeza uongozi wa Rais Samia kwa kuimarisha demokrasia na amani ya kudumu.

DKT NCHIMBI – “UKEREWE KITAJENGWA KIWANDA cha KUCHAKATA SAMAKI na UKAUSHAJI DAGAA”…









