Tarehe 29.10.2025 siku ya Jumatano ni siku muhimu sana katika Taifa letu, ambapo Watanzania watatekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura kwa ajili ya kuchagua Viongozi watakao waongoza katika nafasi ya Urais, Wabunge na Madiwani.
Jeshi la Polisi kupitia taarifa hii, lingependa kuwahakikishia wananchi na wageni watakao kuwa nchini mwetu kuwa hali ya usalama wa nchi ni shwari sana na hakuna tishio lolote la kiusalama linalo weza kufanya shughuli hiyo ya kupiga kura isifanyike kwa amani.
Pia wananchi mnahakikishiwa amani na usalama wa kutosha siku hiyo ya jumatano, hivyo mjitokeze kwa wingi kama mlivyojiandikisha kwenda kupiga kura bila hofu yeyote ile.
Aidha, lina wahakikishia limejipanga vizuri sana kumdhibiti yeyote yule kwa mujibu wa sheria atakaye jitokeza ama kwa makusudi au nia ovu kuvunja sheria za nchi ili kuhatarisha amani ya nchi kwa kisingizio chochote kile siku hiyo ya kupiga kura na baada ya kupiga kura.
Atakaye thubutu kuvunja sheria asilaumu kwa hatua zitakazo chukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria za nchi, kwani elimu imetolewa vya kutosha na kwa muda mrefu.







