
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Hamza Said Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Novemba 3, 2025, imesema Mheshimiwa Johari ataapishwa kesho Jumatano ya Novemba 5, 2025 saa nne asubuhi katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma.









