

Rais wa Marekani, Donald Trump amemchimba mkwara meya mpya (Mteule) wa New York, Zohran Mamdani kwamba anapaswa kuwa na heshima kwa Washington, kwa sababu asipofanya hivyo, hana nafasi ya kufanikiwa.
Akirejea hotuba ya Mamdani ya kukubali ushindi kama Meya wa Jiji la New York, amesema kuwa imejaa hasira dhidi yake na ‘ni hatari sana’.
Baada ya kushinda uchaguzi wa Jumanne, Mamdani alinukuliwa akirusha kijembe kwa Trump, akisema:
“Hivyo nisikie, Rais Trump, ninaposema hivi, ili umfikie yeyote kati yetu, ni lazima upitie kwa wote kati yetu.”
Akihojiwa na mwandishi Bret Baier wa Fox News jana, ikiwa ni siku moja tangu Mamdani ashinde, Trump aliitaja kauli hiyo iliyomlenga kuwa ni kauli hatari sana kwake kuitoa.
Awali, Trump alitishia kutoa kiwango cha chini kabisa cha fedha za shirikisho kwa jiji hilo endapo Mamdani angeibuka mshindi.
Ushindi wa Mamdani kutoka Chama cha Democrat ambao haukutegemewa na wengi, unatajwa kuwa pigo kubwa kwa serikali ya Trump ya Chama cha Republican kwa kupoteza jiji hilo muhimu, na inatajwa kuwa ishara mbaya kwa serikali ya Trump.
MANENO MAZITO ya SHEIKH ALHAD MSIBANI kwa SHEIKH SHARRIF MAJINI – MWILI ULIVYOPATIKANA MUHIMBILI….





