Mh. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa ameketi na Waziri Mkuu mstaafu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa katika hafla ya uapisho Chamwino jijini Dodoma Oktoba 14, 2025
…………….
Na Fullshangwe Media
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 14 Novemba 2025, amezungumza kuhusu utumishi wa Waziri Mkuu mstaafu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, wakati wa hafla ya kumuapisha Mh. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Amesema kuwa kijiti alichokikabidhi kwa Waziri Mkuu mpya kimetoka kwa Waziri Mkuu mstaafu, ndugu yetu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, ambaye amefanya kazi nzuri kufanikisha tunayokumbana nayo leo, tukitambua ujenzi wa shule, vituo vya afya na Hospitali ya Kanda ya Rufaa. Amesema kuwa Majaliwa alikuwa nyuma yake kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri.
Aidha, amebainisha kuwa Majaliwa ni “mfanyakazi mzuri ambaye sina shaka naye, naamini utafuata miguu yake na utaongeza pale unapohisi panahitaji kuongezewa nguvu.” Amesema kuwa kazi aliyoiacha imeweka msingi mzuri wa kuendelezwa.
Rais Samia amesema hayo wakati akisisitiza umuhimu wa kuendeleza kasi ya utendaji na kutekeleza majukumu kama Ilani ya Uchaguzi inavyoelekeza, huku akitambua mchango wa Majaliwa katika kufanikisha hatua ambazo Serikali imekuwa inapitia.







