

Kamati ya Maonesho ya Vitabu Tanzania na Chama cha Wachapishaji Tanzania wanayofuraha kutangaza kwamba maonesho ya 32 ya Kimataifa ya Vitabu Tanzania yatafanyika kuanzia kesho tarehe 21 hadi 26 Novemba 2025 katika Viwanja wa Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo, Kabudi Paramagamba.

Maonesho hayo itawaleta pamoja zaidi ya wadau 30 wa ndani na nje ya nchi katika tasnia ya vitabu, elimu na huduma zinazohusiana, kuanzia wachapishaji, wachapaji, wauza vitabu, shule, vyuo vikuu, taasisi za kitaaluma, idara za serikali pamoja na kampuni zinazotoa huduma.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari jana Mkurugenzi Mkuu wa TLSB, Dkt. Mboni Ruzegea amesema wamezialika nchi mbalimbali ikiwemo Kenya kuwa nchi iliyoalikwa na tunatarajia kukaribisha Wanachama cha Chama cha Wachapishaji Kenya (KPA) inayojumuisha wajumbe wa zaidi ya kampuni 5.
Wakati wa maonesho hayo, vitabu na bidhaa zinazohusiana na shule zitauzwa kwa punguzo katika kampeni ya kukuza masomo ya kudumu, utamaduni wa kusoma na ukuzaji wa taaluma miongoni mwa umma.
Shughuli nyingine zitakazofanyika katika maonesho hayo ni pamoja na uzinduzi wa vitabu, uwekaji saini wa vitabu vya mwandishi na programu ya kusoma kwa watoto.
Programu ya maonesho hayo pia itahusisha mijadala ya kitaalamu ya wadau kuhusu hali ya tasnia ya vitabu barani Afrika na jukumu kuu inayochukua katika kusoma na kuandika, elimu na kukuza urithi wa kitamaduni wa taifa, historia na ushirikiano wa kimataifa.
Maonesho haya yamedhaminiwa na Nyambari Nyagwine Foundation, Meru Oil na wengineo. Maonesho haya yameandaliwa na PATA, TLSB, BAKITA na waandishi na wauza vitabu binafsi.
Naye Katibu wa PATA, Abdullah Saiwaad alisema katika maonesho hayo hakuna kiingilio na kuwakaribisha wote kwa ajili ya kutazama maonesho hayo na kununua vitabu vyote uvitakavyo ambavyo vitakuwepo katika sehemu moja. Alimaliza kusema Saiwaad.






