
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia wahamiaji haramu 14 raia wa Burundi waliokamatwa wakiwa wameingia nchini kinyume cha sheria kwa kutumia magari mawili ya abiria.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, Novemba 23, 2025, wilayani Sengerema wakati akizungumza na vyombo vya habari.
Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa, kukamatwa kwa wahamiaji hao kumetokana na ufuatiliaji wa mienendo ya kihalifu pamoja na uwekaji wa vizuizi barabarani. Katika Kijiji cha Busisi, Tarafa ya Sengerema, wahamiaji haramu 13 walikamatwa Novemba 23, 2025, majira ya saa 7:30 mchana, wakiwa ndani ya gari aina ya Tata lenye namba T 337 DYA, mali ya Chiza Francis Lugubi, mkazi wa Dodoma, linalofanya safari kati ya Kabanga (Ngara, Kagera) na Mwanza.
Wakati wa tukio, dereva wa gari hilo, Jonas Richard, alikimbia na kutokomea, na juhudi za kumtafuta zinaendelea.






