Wito huo ameutoa katika Ukumbi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Kinazini katika ghafla ya makabidhiano ya Ofisi.
Aidha amewashukuru watendaji hao katika kipindi chote Cha utendaji wake Wizarani hapo kwa ushirikiano wao waliyouonyesha hivyo ni vyema kuendeleza zaidi ushirikiano huo ili kufikia malengo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
“Kama tutakwenda vizuri tukafuata maelekezo tuliyopewa basi tutafikia malengo” alisema Waziri Pembe.
Amesema kuwa kazi ya Jamii ni kubwa hivyo ni vyema kujitahidi na kufanya KAZI kwa bidii kwa kufuata Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kufikia dira 2025/2030
Amefahamisha kuwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii ina mambo mengi hivyo ni vyema kufanya KAZI kwa kwa pamoja ili kuweza kusonga mbele na kuleta maendeleo.
Nae Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe, Anna Athanas
Paul ameahidi na kusema kuwa yuko tayari kushirikiana katika kazi ili kufikia lengo.
Aidha amesema kuwa anategemea ushirikiano mzuri Kati yake na watendaji kwani umoja ni nguvu.
Amesema kuwa Ilani ndio nyenzo kwa kila kitu hivyo wataifuata Ilani hiyo ili kufanikisha yale yote yanayotakiwa.
Wakati huo huo Waziri Anna amezindua Kampeni ya siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya watoto na wasichana inayoanza tarehe 25 Novemba hadi 10 Disemba.
Kampeni hiyo yenye Kaulimbiu ya mwaka huu ni: Mitandao Salama ni Haki: Maliza Ukatili wa Kimtandao kwa Wanawake na Watoto ambapo Kaulimbiu hiyo inaakisi changamoto mpya zinazoongezeka kwenye majukwaa ya kidijitali.
Amefahamisha kiwa Ukatili wa kimtandao umekuwa ukiathiri kwa kiwango kikubwa wanawake na watoto, ikiwemo kudhalilishwa, kusambaziwa taarifa binafsi bila ridhaa, kurubuniwa, na vitisho vinavyoathiri afya ya akili, utu na usalama wao.
Aidha amefafanua kuwa maadhimisho hayo yataambatana na shughuli mbali mbali nchini zinalenga kukabiliana na tatizo la ukatili na udhalilishaji.
Waziri Anna ameeleza kuwa kwa kipindi cha mwaka 2023 jumla ya matukio 1,954 ya ukatili na udhalilishaji wa Kijinsia yameripotiwa, mwaka 2024 matukio 1,809 na mwaka 2025 kuanzia Januari hadi Okitoba 2025 jumla ya matukio 1,022 yameripotiwa. Katika matukio yote hayo waathirika wakuu ni wanawake na watoto.
Aidha, watoto wa kike na wakiume wamekua ndio waathirika wakubwa zaidi wa matokeo hayo ya ukatili na udhalilishaji.
Ameongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara imejiwekea vipaumbele vya kukabiliana na tatizo la vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto (GBV/VAC).







