NA Sophia Kingimali.
WAHITIMU 121 wa Chuo cha Ufundi Stadi, Furahika(VETA) wametakiwa kuzingatia maadili wanapokwenda kwenye mafunzo kwa vitendo ili kupata fursa ya kupata ajira.
Pia,wito umetolewa kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanapeleka watoto wao kwenye chuo hicho ili waweze kupata mafunzo ya ufundi stadi ili waweze kujiajili na kuounguza wimbi la vijana waliopo mtaani bila ajira.
Mwenyekiti wa Bodi chuo hicho, Said Said, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Tabata, ametoa wito huo kwa wahitimu hao wakati wa mahafali yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
“Maisha ni mchakato ili ufanikiwe uwe n subira, wavumilivu na kuzingatia maadili ya kazi na kutojiingiza katika uzinzi hali itakayosaidia kuwajengea uaminifu itakayowapa fursa ya kupewa mkataba WA ajira.
“Msiende na mambo mawili mawili yatakayoharibu mwenendo wenu wa maisha, pia mnatakiwa kuangalia kwamba mmetoka katika familia gani, mkienda kufanya tofauti mtawaumiza wazazi wenu kwani wanamatarajio makubwa kwenu baada ya kuhitimu masomo, wakiamini mnakwenda kuwa msaada kwao na familia kwa ujumla,” amesema.
Ameongeza kuwa mwajiri hawezi kumuajiri mtu mwenye tabia za uzinzi, wizi na nyinginezo zisizo na maadili mema.
Amesema kuwepo kwa chuo hicho ni sehemu ya kusapoti juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha watoto wanapata elimu bure kwani chuo hicho kinatoa elimu bure kwa kuchangia hela kidogo kiasi cha shilingi 50,000 ambapo lengo ni kusaidia watoto wanaotoka kwenye kaya maskini.
Kuhusu mahitaji ya chuo, hicho ikiwemo upungufu wa vifaa vya kufundishia, ikiwemo kompyuta, cherehani ameahidi kulifanyia kazi huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali kuweza kujitokeza ili kusaidia kumaliza changamoto hizo.
Naye Mkuu wa Chuo, hicho Aliko Mongele, amesema kuhitimu kwa wahitimu hao katika fani za hotel, Umeme, Bandari, air ticket, ICT, udereva na nyinginezo inatoa fursa ya kusajili wapya kwa muhula mpya utakaonza Januari.
Ameongeza kuwa kwa muhula mpya wa Januari wataanzisha kozi mpya ya ufundi bomba na kutoa wito kwa wazazi kuwapeleka vijana wao kuweza kusoma kozi hiyo na nyinginezo ili kuachana na umasikini na kukaa vijiweni bila ya kuwa na kazi badala yake kujiingiza kwenye makundi maovu.
Pia muhimu wa kozi ya sekretali, Laura Matechi amesema anashukuru kufanikisha ndoto yake na sasa anaamini anakwenda kuitumia ili kufanya vema katika maisha yake na kuondokana na utegemezi ambapo amesema hata akikosa kuajiliwa anaweza kujiajili kwa kufungua stationary yake na kutoa huduma.
Pia muhitimu, Moses Victor, ametoa wito kwa vijana ambao wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto kadhaa wajitokeze kwenye Chuo hicho ili wapate elimu bure bila malipo ingawa wanacholipi na ada ya mtihani 50,000 na fomu pekee.







