Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh.patrobas Katambi akizungumza kwenye mahafari ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Mwanza
Wahitimu wakiwa katika eneo la sherehe za mahafali. 
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE kampasi ya Mwanza Profesa Edda Lwoga akizungumza kwenye mahafali ya 60 ya chuo hicho yanayofanyika kwa mara ya18 katika kampasi ya hiyo. 
Baadhi ya Wahitimu wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Mwnza.
…………….
Na Hellen Mtereko,Mwanza
Wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Mwanza wameaswa kuwa waadilifu wanapokwenda kwenye jamii hatua itakayosaidia kutatua changamoto zilipo kwa weledi.
Hayo yamebainishwa Desemba 06, 2025 na Naibu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe.Patrobasi Katambi kwaniaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mh.Judithi Kapinga kwenye mahafali ya 60 ya chuo hicho ambapo yanafanyika kwa mara ya 18 katika kampasi ya Mwanza.
Amesema changamoto za kiuchumi,kijamii na kimazingira zipo Kila sehemu hivyo wanatakiwa kuwa waadilifu kwa kutumia elimi waliyoipata ili iweze kuleta matokeo yenye tija.
“Nendeni mkatoe mchango wa mawazo kwenye jamii kwani mawazo yenu yanaweza kuleta mabadilko makubwa kwenye maendeleo ya Taifa”,
Aidha, ameeleza kuwa maendeleo hayaji hivi hivi Bali Kwa mchakato unaohitaji kujitoa,kujinyima kwa faida ya kesho.
“Kama wahenga wasemavyo mchumia juani hulia kivulini hij inaenda kuthibitisha kwamba katika kipindi chote ambacho mlikuwa katika masomo yatawapelekeeni kufikia kivulini kwa maana ya kuwahudumia watanzania kwakutumia taaluma mliyoipata”, amesema Katambi
Amesema uaminifu na uzalendo ndio nguzo kuu ya mafanikio hivyo amewaomba wahitimu kuendelea kuwa waaminifu katika kutekeleza majjkumu ya nchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Mwanza Profesa Edda Lwoga, amesema jumla ya wahitimu 854 wamehitimu katika ngazi mbalimbali kuanzia Cheti,Astashahada,Stashahada.






