

Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Harmonize, ameibua shangwe kubwa baada ya kutangaza wazi kuwa amerejea katika uhusiano na Kajala Frida usiku wa kuamkia leo Desemba 26, 2026 wakati akifanya sho0 Zanzibar.
Tukio hilo lililovutia mashabiki wengi, Harmonize alimuita Kajala jukwaani na kumtuza maneno ya upendo, akisisitiza kuwa:
“Kajala ndiye mwanamke mrembo zaidi kuwahi kumuona duniani.”
Mashabiki waliopiga kelele za furaha wamesherehekea tukio hilo, wengi wakilitafsiri kama kurasa mpya katika uhusiano wao ambao hapo nyuma uliwahi kupita kwenye misukosuko.
Hadi sasa, wawili hao bado hawajaweka wazi hatua zao zinazofuata, lakini mashabiki wanaonekana kufurahia kuona amani na furaha ikirejea kati yao wakisema ndoa inakuja.
The post Wamerudiana! Harmonize Amshangaza Kajala Jukwaani, Zanzibar Yazizima appeared first on Global Publishers.







