MKUU wa mkoa wa Arusha ,CPA Amos Makalla akizungumza kwenye halfa hiyo jijini Aruaha leo
Happy Lazaro,Arusha
Arusha. MKUU wa mkoa wa Arusha ,CPA Amos Makalla amekabithi hundi yenye thamani ya shs 2.3 bilioni ikiwa ni fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu wa AFCON 2027.
Ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati akizungumza katika halfa ya kukabithi hundi hiyo kwa wananchi hao hafla iliyofanyika katika viwanja hivyo jijini Arusha .
CPA Makalla amesema kuwa,mradi huo hadi kukamilika utagharimu kiasi cha shs 340 bilioni ambapo mradi unatarajiwa kukamilika julai mwakani .
“Tunaomba sana uwanja huu ukamilike kwa wakati ili kupisha mashindano ya AFCON yatakayofanyika mwaka 2027 na kuhakikisha yale yote yanayoonekana Morocco yaonekane huku kwetu Tanzania pia .”amesema CPA Makalla.
Makalla amesema kuwa, mradi umefikia asilimia 70 hadi sasa hivi na mkandarasi yupo vizuri kwani anafanya kazi kwa wakati na kwa spidi inayotakiwa .
“Naomba sana mhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati na kusiwepo na excuse yoyote ya kuchelewesha mradi huu tunaomba sana muwe makini kwani macho yote yanaangalia huu mradi hivyo ongezeni umakini katika kazi yenu nawaomba sana .”amesema .
Ameongeza kuwa ,uwepo wa mradi huo kwetu ni fursa kubwa kwa wana Arusha kwani yale yote yanayoonekana Morocco yatakuja kuonekana hapa kwetu na kutaleta fursa nyingi za utalii wa michezo .
Kwa upande wake Afisa mipangomiji wa jiji Doroth Absalom amesema kuwa ,eneo lote la mradi huo ni hekari 83 ,ambapo wananchi 12 ndio wanalipwa fidia ambapo kati ya hao wananchi 7 walishalipwa na halmashauri ya jiji ambapo wengine 5 ndio wanalipwa na wizara ya utamaduni Sanaa na michezo .
Naye Msimamizi wa mradi huo QS Dennis Mtemi amesema kuwa ,mradi upo ndani ya muda na unatarajiwa kukamilika muda uliopangwa .
“Tunaishukuru sana serikali kwa kutupa ushirikiano wa kutosha na tunaahidi kumaliza mradi ndani ya muda uliopangwa japo kuna changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara tunaomba serikali iharakishe mchakato wa miundombinu hiyo ili kuondokana na changamoto hiyo.”amesema .






