Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akifurahia jambo na Mama Anna Mkapa (kulia), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa wakati alipomtembelea nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 06 Januari, 2026.
Na. Veronica Mwafisi-Dar es salaam
Tarehe 06 Januari, 2026
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amewatembelea na kuwajulia hali Mama Maria Nyerere, mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam na Mama Anna Mkapa, mke wa Hayati Benjamin William Mkapa nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam leo January 6, 2026.
Mhe. Kikwete amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anathamini sana mchango wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa waliomtangulia na ataendelea kusimamia na kutunza familia hizo kwa mujibu wa Katiba na Sheria zilizowekwa.
Aidha, Mhe. Ridhiwani amesema, kuwatembelea na kuwajulia hali wake hao wa Viongozi Wastaafu ni moja ya majukumu yake ambayo anayatekeleza kwa lengo la kuwajulia hali, kusikiliza changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi kwa mujibu wa Katiba na Sheria zilizowekwa.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amesema ofisi hiyo itafanyia kazi maoni na ushauri uliotolewa na wajane hao.
Aidha, Mama Maria Nyerere amemshukuru Mhe. Kikwete kwa kupata nafasi ya kumtembelea na kumjulia hali na amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali familia yake wakati wote pasipo kuchoka.
Naye, Mama Anna Mkapa ameishukuru ofisi hiyo kwa kufuatilia kwa karibu masuala yanayowahusu na kuyatafutia ufumbuzi.
Mama Anna Mkapa (wa kwanza kulia), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa akimsindikiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) wakati Waziri huyo akiondoka baada ya kumtembelea nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 06 Januari, 2026. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi.
Mama Anna Mkapa (wa kwanza kulia), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa akimsindikiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) wakati Waziri huyo akiondoka baada ya kumtembelea nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 06 Januari, 2026. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mama Anna Mkapa (katikati), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa wakati Waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam leo tarehe 06 Januari, 2026. Wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi na wengine ni Wakurugenzi kutoka katika ofisi hiyo.





