

Uongozi wa Young Africans Sports Club (Yanga SC) unampongeza Mdhamini na Mfadhili wa Klabu hiyo, GSM, kwa kumuozesha binti yake, Fatma Ghalib Said Mohammed, katika hafla ya ndoa iliyofanyika jana, Januari 10, 2026, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo ya ndoa ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azan Zungu.

Wageni wengine mashuhuri waliohudhuria ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa Kassim, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, Waziri wa Maji, Awesu, pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamiss Mwinjuma (Mwana FA).
Uongozi wa Yanga SC unaendelea kumtakia GSM, familia na wanandoa heri, baraka na maisha yenye amani, upendo na mafanikio tele.

The post Yanga Yampongeza GSM Kwa Harusi ya Binti Yake Jijini Dar appeared first on Global Publishers.





