

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu picha mjongeo inayosambazwa katika mitandao ya kijamii ikionesha Askari Polisi akipambana na mtu mmoja huku akiwa na silaha ya moto.
Taarifa sahihi ni kuwa, mnamo Januari 15, 2026 majira ya saa nane mchana katika Benki ya CRDB tawi la Sirari – Tarime, mtu aitwaye JOHN KOHE AMOSI, Mkuru, Mkazi wa Kijiji cha Sokoni – Sirari, alifika katika benki hiyo na kuingia ndani moja kwa moja hadi kwa mtoa huduma wa benki (bank teller) kama mtajwa huku akiwa amebeba begi dogo na kumwamuru kwa nguvu mtoa huduma ampe fedha bila kufuata taratibu za kibenki.
Hali hiyo ilisababisha wasiwasi ndani ya benki na kulazimu Askari Polisi waliokuwa lindo nje ya benki hiyo wajulishe na wakamfuata mtu huyo na kumtaka atoke nje na alitii amri hiyo.
Wakati anasindikizwa na Askari kutoka nje ghafla alimvamia askari kwa lengo la kumpora silaha kwa kupambana na askari, hata hivyo askari waliifanikiwa kumdhibiti na kumtoa nje ya benki bila kutumia silaha pamoja na kitendo alichofanya.
Aidha, uchunguzi wa awali ulibaini kuwa, mtu huyu hana akaunti kwenye benki ya CRDB. Uchunguzi wa kina bado unaendelea ili kubaini nia ya mtu huyo ilikuwa ni nini na alikuwa anasukumwa na kitu gani hadi kufanya aliyoyafanya ili hatua zingine za kisheria zichukuliwe.
The post CCTV Camera Zilivyonasa Jamaa Akipigana na Askari Polisi – Video appeared first on Global Publishers.





