

Shambulio la droni dhidi ya msafara wa misaada katika jimbo la Kordofan Kaskazini mwa Sudan limemuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine kadhaa huku asasi za kiraia nchini humo zikiwalaumu wanamgambo.
Msafara huo ulikuwa unaelekea katika eneo la karibu na El-Obeid, mji unaodhibitiwa na jeshi lakini ambao umekuwa ukizingirwa na vikosi vya wanamgambo wa RSF kwa mwaka mmoja sasa.
Mratibu wa misaada kwenye Umoja wa Mataifa Denise Brown, amesema baada ya kutembelea El-Obeid alishuhudia athari za shambulizi hilo zilizojumuisha kuchomwa kwa malori ya misaada.
Alielezea wasiwasi mkubwa juu ya shambulio hilo na akatoa wito wa kuzingatia ulinzi wa wafanyakazi wa mashirika ya misaada, mali na bidhaa.
Shirika la haki za binadamu nchini humo liitwalo Emergency Lawyers, limethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo na kulihusisha moja kwa moja kundi la RSF.
The post Msafara wa Misaada Washambuliwa Kwa Drone, Mmoja Afariki appeared first on Global Publishers.




